Mpya HR & Payroll sasa ipo tayari

Jua faida yako, madeni na stoo kila siku.

InchFam Books inaweka mauzo, manunuzi, matumizi, stoo, benki, mishahara na ripoti za kihasibu sehemu moja. Imejengwa kwa ajili ya biashara na taasisi za Tanzania.

Onboarding ya msingi ni bure · Msaada kwa Kiswahili
  • Maduka
  • Wholesalers
  • Taasisi za Kidini
  • Accountants
  • Garage
  • Vituo vya mafuta
Bidhaa ya InchFam Technologies Limited
Owner Dashboard ya InchFam Books ikionyesha mapato, matumizi, madeni, salio la cash na benki, faida, na chati ya mapato dhidi ya matumizi
TZS 20,000kwa mwezi, Core Accounting
Modules 5za sekta, ongeza unazohitaji tu
P&L, Balance SheetTrial Balance na General Ledger tayari
Kwenye simuna kompyuta, bila kusakinisha
Tunachotatua

Kama umewahi kusema mojawapo ya haya, InchFam Books ni kwa ajili yako

Kila tatizo hapa chini lina sehemu ya mfumo iliyojengwa mahsusi kulitatua.

Tatizo
Jinsi InchFam Books inavyolitatua
“Wateja wanadaiwa, lakini sijui jumla ni kiasi gani wala nani amechelewa.”
Kila ankara inaingia kwenye akaunti ya mteja. Unaona salio la kila mteja, unampa statement yake, na unawatumia SMS za kuwakumbusha.Sales Invoices · Customer Receipts · Customer Statements · Bulk SMS
“Nauza kila siku, lakini mwisho wa mwezi sioni faida.”
Mauzo, manunuzi na matumizi vinaingia kwenye vitabu vya hesabu moja kwa moja. Profit & Loss na Balance Sheet ziko tayari wakati wowote.Business & Accounting Reports · Owner Dashboard
“Bidhaa zinapungua stoo na sijui zinakwenda wapi.”
Stoo inapungua kila unapouza na kuongezeka unaponunua. Marekebisho ya stoo yanahitaji ruhusa maalum na yanaacha kumbukumbu ya aliyeyafanya.Inventory Management · Stock Adjustments
“Pesa za droo, benki na Lipa Namba hazilingani na hesabu.”
Kila uhamisho wa pesa kati ya akaunti unarekodiwa, na unalinganisha salio la mfumo na taarifa ya benki kupitia bank reconciliation.Cash & Bank Transfers · Bank Reconciliation
“Natoa quotation, kisha naiandika upya kuwa ankara kwa mkono.”
Tuma quotation kwa mteja. Akikubali, igeuze kuwa invoice kwa kubofya, na utoe delivery note kutoka invoice hiyo hiyo.Sales Quotations · Proforma Invoices · Delivery Notes
“Nikiwa mbali na biashara, sijui kilichotokea leo.”
Fungua dashboard kwenye simu uone mauzo, madeni na salio. Kila mfanyakazi ana My Day Report, na kila kitendo kina jina la aliyekifanya.Owner Dashboard · My Day Report · Roles & Permissions
Core Accounting · TZS 20,000/mwezi

Msingi wa uhasibu wa biashara, sehemu 15 ndani ya kifurushi kimoja

Core Accounting inafaa kwa maduka, wholesalers, distributors, biashara za huduma na biashara yoyote inayohitaji kumbukumbu sahihi za kifedha.

Mauzo na Wateja

Kutoka quotation hadi pesa mkononi.

Sales Management

Usimamizi wa Mauzo

Toa ankara za mauzo ya bidhaa na huduma, pokea malipo ya wateja, andaa proforma invoices na delivery notes, na toa customer statement yenye mauzo, malipo na deni.

Unafuatilia mauzo, mapokezi na madeni ya kila mteja.

Sales Quotations

Makadirio ya Mauzo

Tengeneza na tuma quotations, fuatilia zilizokubaliwa au kukataliwa, na geuza iliyokubaliwa kuwa invoice.

Inarahisisha kuuza kwa oda na makubaliano ya bei.

Customers

Usimamizi wa Wateja

Sajili wateja, simamia taarifa zao, fuatilia miamala yao, na rekodi fedha wanazolipa mapema kama deposits.

Advance za wateja hazichanganyiki na mauzo.

Other Income

Mapato Mengine

Rekodi mapato yasiyotokana na mauzo ya kawaida, kama kodi ya pango, kamisheni au huduma za ziada.

Mapato yote ya biashara yanaonekana sehemu moja.

Bulk SMS

SMS kwa Wateja

Tuma SMS kwa wateja wako, ikiwemo jumbe za kuwakumbusha madeni yao moja kwa moja kutoka kwenye orodha ya wadaiwa.

Madeni yanalipwa haraka bila kupiga simu moja moja.

Manunuzi na Matumizi

Kila shilingi inayotoka ina kumbukumbu.

Purchases

Usimamizi wa Manunuzi

Rekodi purchase invoices, ongeza landed costs (usafiri, ushuru, clearing) kwenye gharama ya bidhaa, lipa wasambazaji na toa supplier statements.

Unajua gharama halisi ya kila bidhaa na deni lako kwa suppliers.

Suppliers

Usimamizi wa Wasambazaji

Sajili na simamia taarifa za wasambazaji wa bidhaa na huduma pamoja na historia ya miamala yao.

Hakuna kulipa mara mbili wala kusahau deni.

Expenses

Usimamizi wa Matumizi

Rekodi na simamia matumizi kama kodi, umeme, maji, usafiri na gharama nyingine za uendeshaji, kwa kila mlipwaji.

Unaona matumizi madogo madogo yanayokula faida.

Stoo na Fedha

Unajua kilichopo stoo na kwenye kila akaunti.

Inventory Management

Usimamizi wa Bidhaa

Sajili bidhaa na huduma, ingiza opening stock, fuatilia current stock, fanya stock adjustments kwa ruhusa maalum, na pata inventory reports.

Unajua bidhaa zilizopo, zilizopungua na thamani ya stoo.

Cash Management

Usimamizi wa Fedha

Rekodi uhamisho wa fedha kati ya cash, benki na mobile money, na linganisha kumbukumbu za benki na mfumo kupitia bank reconciliation.

Unajua fedha zilizopo kila akaunti, kwa uhakika.

Loans

Usimamizi wa Mikopo

Rekodi mikopo na miamala yake yote: mapokezi, marejesho na gharama zake.

Fedha za mkopo hazionekani kama mapato ya biashara.

Owner Transactions

Miamala ya Mmiliki

Rekodi fedha ambazo mmiliki anachukua kwenye biashara kwa matumizi binafsi (Owner Withdrawals).

Fedha za biashara na za mmiliki zinatenganishwa.

Ripoti na Mipangilio

Hesabu zilizo tayari kwa maamuzi na kwa mhasibu.

Business & Accounting Reports

Taarifa za Biashara na Uhasibu

Mauzo na manunuzi, madeni ya wateja na wasambazaji, stoo, Profit & Loss, Balance Sheet, Trial Balance, General Ledger, Cash & Bank Summary na My Day Report.

Maamuzi yako yanategemea takwimu, si makisio.

Owner Dashboard

Dashboard ya Mmiliki

Mapato, matumizi, madeni, salio la cash na benki na faida kwenye skrini moja, kwa siku, wiki au mwaka mzima.

Unaona mwenendo wa biashara wakati wowote.

Accounting Setup

Mipangilio ya Uhasibu

Simamia Chart of Accounts, Fiscal Years, Tax Configuration (kama VAT) na Opening Balances.

Msingi sahihi wa kumbukumbu, tayari kwa mhasibu na ukaguzi.
Ndani ya mfumo

Angalia skrini na nyaraka halisi za InchFam Books

Picha zote ni za kampuni ya mfano (Demo Company). Bofya picha kuiona kwa ukubwa.

Owner DashboardMapato, matumizi, madeni, salio na faida kwa kipindi chochote, pamoja na mchanganuo wa matumizi.
Ripoti ya MauzoMauzo, punguzo, pesa zilizokusanywa na madeni yaliyobaki, mwezi kwa mwezi.
Cash & Bank SummaryPesa iliyoingia na kutoka, na salio la kila akaunti: cash, benki na mobile money.
Additional Modules · TZS 10,000/mwezi kila moja

Ongeza uwezo maalum wa shughuli zako juu ya Core Accounting

Badala ya kutumia mifumo mingi tofauti, unatumia msingi mmoja wa uhasibu na kuongeza module moja au zaidi. Kila module inaingiza miamala yake kwenye vitabu vyako vya hesabu moja kwa moja.

01

HR & Payroll

Kwa biashara na taasisi zenye wafanyakazi wanaolipwa mshahara kila mwezi.

+ TZS 10,000kwa mwezi · 100,000 kwa mwaka
ChangamotoKuandaa mishahara, makato na malipo ya kisheria kila mwezi kwa Excel kunachukua muda, kunaleta makosa, na gharama hizo haziingii kwenye vitabu vya hesabu.
SuluhishoSajili wafanyakazi, idara na nafasi zao. Andaa payroll, irekebishe, iidhinishe na ilipe, kisha rekodi malipo ya kisheria (statutory). Gharama zote zinaingia kwenye vitabu moja kwa moja.
EmployeesDepartmentsPositionsPayroll RunsPayroll ApprovalEmployee PayrollPayroll SettingsStatutory PaymentsPayroll Reports
02

Religious Institutions

Kwa taasisi za kidini na nyingine zinazokusanya michango kutoka kwa wanachama au waumini.

+ TZS 10,000kwa mwezi · 100,000 kwa mwaka
ChangamotoSadaka, zaka, michango ya ujenzi na ahadi zinaandikwa kwenye madaftari, waumini hawajui michango yao, na fedha za mfuko maalum zinachanganyika na matumizi ya kawaida.
SuluhishoSajili wanachama, familia na vikundi; rekodi michango kwa aina na mipango; fuatilia ahadi (pledges); tenganisha mifuko maalum na matumizi yake. Wanachama wanaona michango yao kwa login zao.
MembersMember LoginsFamiliesGroupsMilestonesContributionsContribution TypesContribution PlansPledgesRestricted FundsFund DisbursementsContribution ReportsMember SMSOnline Payments (ClickPesa)

Malipo ya mtandaoni kupitia ClickPesa: wanachama wanalipa michango moja kwa moja kwenye mfumo. Huduma hii inapatikana kwa module hii pekee.

03

Accountant Desk

Kwa accountants na CPA wanaosimamia taarifa za kifedha na mafaili ya kodi ya wateja wengi.

+ TZS 10,000kwa mwezi · 100,000 kwa mwaka
ChangamotoTaarifa za wateja zinakuja kwa WhatsApp na karatasi, na kuandaa financial statements na returns kila mwaka ni kazi ya kurudia.
SuluhishoKila mteja ana faili la kodi kwa kila mwaka. Mfumo unatengeneza financial statements, tax computation na return preparation, na unahifadhi working papers pamoja na audit trail.
ClientsTax FilesBusiness SummaryFixed Assets ScheduleTax SchedulesFinancial StatementsStatement AdjustmentsTax ComputationTax Rules & RatesReturn PreparationWorking PapersAudit Trail
04

Maintenance

Kwa computer na phone repair shops, gereji za magari na pikipiki, na wauzaji wa spare parts wanaotoa huduma za matengenezo.

+ TZS 10,000kwa mwezi · 100,000 kwa mwaka
ChangamotoVifaa vingi vinapokelewa, lakini hujui kazi ipi iko hatua gani, vipuri vipi vimetumika, wala kama kazi ilileta faida.
SuluhishoFungua job card kwa kila kifaa, tuma quotation, toa vipuri kutoka stoo, kisha tengeneza invoice kutoka kazi yenyewe na uone faida ya kila kazi.
DevicesJob CardsQuotationsParts IssueJob InvoicesOpen Jobs ReportJob Profit Report
05

Fuel Management

Kwa vituo vya mafuta vinavyosimamia pampu, wahudumu na zamu za kazi.

+ TZS 10,000kwa mwezi · 100,000 kwa mwaka
ChangamotoLita zilizouzwa na pesa zilizoletwa na mhudumu hazilingani, na upotevu wa tanki unagundulika kuchelewa.
SuluhishoFungua na funga kila zamu kwa kila pampu na mhudumu, thibitisha makusanyo, na pima matenki (dipping) kulinganisha stoo halisi na ya mfumo.
Pump ShiftsPumps & NozzlesAttendantsFuel TypesTanksTank DippingFuel Reports

Wafanyakazi wanafanya kazi, wewe unabaki na udhibiti.

Mpe cashier au karani mfumo bila hofu. Kila mtumiaji anapewa ruhusa za vitendo anavyohitaji tu.

Ruhusa kwa kila kitendo

Zaidi ya ruhusa 300 za kuchagua moja moja. Cashier anaweza kutoa ankara bila kuweza kuifuta au kuireverse.

Vitendo nyeti vinaonyeshwa wazi

Post, reverse, void, delete, approve na close vinawekwa alama ya tahadhari ili ujue unachokitoa.

Historia haifutiki kimya kimya

Muamala uliokosewa unarekebishwa kwa reverse au cancel, hivyo kumbukumbu inabaki. Usimamizi wa watumiaji na roles ni wa admin pekee.

Bei za InchFam Books

Lipia Core Accounting, kisha ongeza modules unazohitaji tu

Core Accounting ni TZS 20,000 kwa mwezi au TZS 200,000 kwa mwaka. Kila module inayoongezwa ni TZS 10,000 kwa mwezi au TZS 100,000 kwa mwaka. Chagua hapa chini uone bei yako.

Core AccountingMauzo, manunuzi, stoo, matumizi, benki, ripoti, SMS
Bei yako
TZS200,000
kwa mwaka
    Omba Quotation kwa WhatsApp

    Jedwali la bei

    KifurushiKwa Mwezi (TZS)Kwa Mwaka (TZS)
    Core Accounting20,000200,000
    Core + Module 130,000300,000
    Core + Modules 240,000400,000
    Core + Modules 350,000500,000
    Core + Modules 460,000600,000
    Core + Modules 570,000700,000

    Mifano ya bei kwa mwaka

    • Duka au wholesalerCore Accounting pekee
      TZS 200,000
    • Biashara yenye wafanyakaziCore + HR & Payroll
      TZS 300,000
    • Taasisi za kidini Core + Religious Institutions
      TZS 300,000
    • Accountant au CPACore + Accountant Desk
      TZS 300,000
    • Garage au repair shopCore + Maintenance
      TZS 300,000
    • Petrol stationCore + Fuel Management
      TZS 300,000
    Training na kuanzisha mfumo

    Hatukuachi peke yako baada ya kujisajili

    Tunakusaidia kuanza kutumia mfumo kwa ufanisi, kulingana na mahitaji yako.

    Basic Onboarding

    Utambulisho wa awali wa mfumo na maelekezo ya kuanza kuutumia.

    Bure bila malipo ya ziada

    Online Training

    Mafunzo ya kina kupitia mtandao, session ya hadi saa 2.

    TZS 50,000 / session

    Onsite Training

    Mafunzo kwenye eneo lako, hadi saa 6 kwa siku. Usafiri na malazi, inapohitajika, hulipiwa tofauti kwa makubaliano.

    TZS 100,000 / siku

    Data Setup & Configuration

    Tunaandaa bidhaa, wateja, suppliers, Chart of Accounts na Opening Balances zako.

    Kwa makubaliano kulingana na data

    Jinsi ya kuanza

    Hatua tatu kutoka madaftari hadi hesabu zilizo tayari.

    1. Tueleze biashara yako

      Wasiliana nasi na eleza aina ya biashara au taasisi yako.

    2. Ona demo na ushauri

      Tunakushauri Core na Modules zinazokufaa na kukuonyesha mfumo kupitia demo.

    3. Lipa na anza kutumia

      Unapokea quotation na utaratibu wa malipo. Baada ya malipo, mfumo unaandaliwa na unapata maelekezo ya kuanza.

    Maswali

    Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

    Swali lako halipo hapa? Tuulize kwa WhatsApp.

    Naweza kuuona mfumo kabla ya kulipa?

    Ndiyo. Tunakuonyesha mfumo kupitia demo na kukushauri Core na Modules zinazofaa biashara yako kabla hujalipa chochote.

    Je, ninahitaji kusakinisha programu?

    Hapana. InchFam Books inafanya kazi kupitia browser kwenye kompyuta, tablet au simu. Unaingia na kuanza kazi.

    Naweza kuanza na Core kisha kuongeza module baadaye?

    Ndiyo. Unaanza na Core Accounting na kuongeza module moja au zaidi biashara yako inapokua. Kila module ni TZS 10,000 kwa mwezi au TZS 100,000 kwa mwaka.

    Nikilipa kwa mwaka naokoa kiasi gani?

    Bei ya mwaka ni sawa na miezi 10. Kwa Core Accounting unalipa TZS 200,000 badala ya TZS 240,000, hivyo unaokoa TZS 40,000. Kila module unaokoa TZS 20,000 kwa mwaka.

    Mtanisaidia kuingiza bidhaa, wateja na opening balances?

    Ndiyo. Huduma ya Data Setup & Initial Configuration inaandaa bidhaa, wateja, suppliers, Chart of Accounts na opening balances zako. Gharama inategemea ukubwa wa data na kazi.

    Malipo ya mtandaoni kupitia ClickPesa yanapatikana kwa nani?

    Kwa sasa ClickPesa inapatikana kwa module ya Religious Institutions pekee, ambapo wanachama na waumini hulipa michango yao moja kwa moja kwenye mfumo.

    Wafanyakazi wangu wanaweza kufuta mauzo au kubadilisha stoo?

    Hapana, isipokuwa umewapa ruhusa hiyo. Kila mtumiaji anapewa role yenye vitendo maalum, na vitendo nyeti kama reverse, delete na stock adjustment vinahitaji ruhusa yake.

    Omba demo au quotation

    Jaza fomu, nayo itafungua WhatsApp ikiwa na ujumbe tayari kwa timu yetu. Tunajibu kwa Kiswahili au Kiingereza.

    Simu / WhatsApp+255 752 659 255
    OfisiMoshi, Tanzania
    Modules unazovutiwa nazo (si lazima)
    Hakuna taarifa inayohifadhiwa kwenye ukurasa huu. Ujumbe unatumwa kupitia WhatsApp yako.